Galatians 5:1-6

Uhuru Ndani Ya Al-Masihi

1 aAl-Masihi alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.

2 bSikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Al-Masihi hatawafaidia chochote. 3 cNamshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 4 dNinyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Al-Masihi, mko mbali na neema ya Mungu. 5 eKwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 6 fKwa maana ndani ya Al-Masihi Isa, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

Copyright information for SwhKC